Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Harakati ya “Utamaduni wa Kuunga Mkono Muqawama” iliandaa kikao chenye anuani “Lebanon Ina Nguvu Zaidi Kupitia Uhusiano Wake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Katika Mwelekeo wa Kurekebisha Mahusiano ya Udugu”, kilichofanyika katika Hoteli ya Canaan mjini Baalbek.
Waliohudhuria katika kikao hicho ni pamoja na Hussein Al-Hajj Hassan, Mkuu wa Kambi ya Wabunge wa Baalbek bungeni; Hamad Hassan, Waziri wa zamani; Jamal Al-Taqsh, Mbunge wa zamani; Mohammad Reza Mortazavi, Mshauri wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon; Ali Hijazi, Katibu Mkuu wa Chama cha Al-Rayah Al-Watani; mwakilishi wa Harakati ya Amal, Hajj Ali Karkaba; mwakilishi wa Chama cha Kisoshalisti cha Kitaifa cha Syria, Hussein Al-Hajj Hassan; Ahmad Al-Tufaili, Meya wa Baalbek; Wael Adwan, kiongozi wa Harakati ya Hamas; Ata Sahwil, kiongozi wa Harakati ya Jihad ya Kiislamu; Sheikh Khidr Al-Kabash, Mkuu wa Harakati ya Al-Irtiqaa; Sheikh Hussein Ghubris, Mkuu wa Mahusiano ya Umma wa Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu; Sheikh Abdullah Al-Jabri, Katibu Mkuu wa Harakati ya Ummah ya Lebanon; Hussein Nasrallah, Katibu Mkuu wa Atabatu Tukufu ya Haram ya Sayyida Khawlah (as), pamoja na idadi ya viongozi wa kisiasa, kidini, kijamii na wanazuoni wa dini.
Hussein Al-Hajj Hassan
Katika hotuba yake, Hussein Al-Hajj Hassan aliwataka viongozi wa Lebanon kuachana na msimamo wao wakati bado kuna mwanya wa matumaini, na wazinduke kabla hawajachelewa na kabla hawajaitia nchi katika fitina, hata hivyo, alisema kana kwamba hakuna anayesikiliza.
Aliwataka viongozi hao warekebishe mahusiano yao na wananchi wao kwa ajili ya kuimarisha umoja wa Lebanon, kwani damu za mashahidi bado hazijakauka, lakini wao wamejikuta wakijitupa mikononi mwa adui. Aidha, alisema kuwa askari, maafisa na vikosi vya usalama vya serikali pamoja na vikosi vya ulinzi wa kiraia walilengwa na kuuawa kishahidi, huku viongozi hao wakipoteza haki zao walipoamua kuachana na haki ya kuwafikisha wahusika mbele ya vyombo vya sheria.
Al-Hajj Hassan pia aliwataka viongozi warekebishe mahusiano yao na Iran pamoja na viongozi wenye busara wa Lebanon, akiwemo Rais wa Bunge Nabih Berri, Walid Jumblatt, Gebran Bassil, Suleiman Frangieh, Talal Arslan, pamoja na wabunge wengine ambao kisiasa hawako upande wao lakini wameikosoa serikali kwa uwazi na kwa ukali.
Aliongeza kusema: “Mmefunga suala la kujiondoa kwa Israel, kurejea kwa wakimbizi, ujenzi upya wa nchi na ukombozi wa ardhi na suala la kunyang’anywa silaha muqawama, hili ni jambo ambalo ninyi, mnaojiita watetezi wa mamlaka ya taifa huku mkiitishia Lebanon fitina, hamwezi kulitekeleza, mliapa kuilinda Katiba, lakini tangu Tom Barrack alipowadhalilisha waandishi wa habari katika Ikulu ya Rais, na tangu aliposema kwamba Lebanon ni taifa lililoshindwa na kwamba litaunganishwa na Syria, na tangu aliposema kuwa hawataki kulipa jeshi silaha kwa sababu liko upande wa muqawama, mmezoea udhalili, utegemezi na ufuasi. Wananchi ndio wanaopaswa kuhukumu jambo hili, huku ndege zisizo na rubani zikizunguka kila pembe ya Lebanon na kuruka juu ya Beirut, Dhahiya na Bonde la Bekaa.”
Aidha alisema kuwa; makubaliano ya Iran yanailazimisha Israel kujiondoa ndani ya siku 60, lakini viongozi wa Lebanon hawakuwaambia wananchi ni muda gani adui amepewa kujiondoa, wala kipindi cha majaribio ni cha muda gani.
Mwishoni mwa hotuba yake alisema: “Ukiyasoma Makubaliano ya Washington ni msiba, na usipoyasoma ni msiba mkubwa zaidi, kwa sababu makubaliano hayo yanailazimisha Lebanon kutekeleza wajibu mbalimbali, ilhali hayamwekei adui Muisraeli wajibu wowote.”

Sheikh Khidr Al-Kabash: Lebanon Haitakuwa ya Marekani Wala ya Israel
Sheikh Khidr Al-Kabash, Mkuu wa Harakati ya Al-Irtiqaa, pia alisisitiza kupinga “Makubaliano ya Washington” na hatua yoyote ya kuhalalisha uhusiano na Israel, aidha, alitoa wito wa kurekebishwa kwa mahusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambayo kwa mujibu wake daima imekuwa na inaendelea kuwa ngome ya kutetea kadhia ya Palestina na haijawahi kuiacha.
Akilihutubia viongozi wa Lebanon alisema: “Lebanon haitakuwa ya Marekani wala ya Israel, apende asipende yeyote.”
Mshauri wa Utamaduni wa Iran
Kwa upande mwingine, Mohammad Reza Mortazavi, Mshauri wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon, alisisitiza kwamba; Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina misingi isiyobadilika ambayo haitaiacha katika msimamo wake kuhusu Lebanon, hasa baada ya Beirut na Dhahiya kulengwa na mashambulizi. Alikumbusha kuwa Iran iliijumuisha Lebanon katika kifungu cha kwanza cha makubaliano, na kwamba madai yanayosambazwa na baadhi ya watu kuwa muqawama wa Lebanon unafanya kazi kwa niaba ya Iran si ya kweli.
Akieleza kwamba kushikamana na chaguo la muqawama ndiyo njia kuu ya kuikomboa ardhi na kurejesha haki, alisema: “Tutasherehekea pamoja nanyi ukombozi wa tatu, si katika Bint Jbeil au Baalbek pekee, bali ndani ya Lebanon yote.”
Mortazavi alisisitiza kuwa; Iran inaunga mkono uhuru wa Lebanon, umoja na muqawama wake halali dhidi ya uvamizi wa Kizayuni, na kwamba haitaiacha Lebanon peke yake, aliongeza kuwa: Lebanon itakuwa sehemu kuu katika mazungumzo yoyote yajayo, na Iran itaendelea kusimama pamoja na wananchi wake, huu ndio ujumbe wa Kiongozi wa Muqawama wa Kiislamu Imam Sayyid Ali Khamenei pamoja na Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, ambao wote wanasisitiza kuendelea kusimama pamoja na nguvu za muqawama nchini Lebanon.
Sheikh Hussein Ghubris
Naye Sheikh Hussein Ghubris, Mkuu wa Mahusiano ya Umma wa Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu, alihoji sababu na siri ya uadui dhidi ya Iran, akisisitiza kwamba hakuna mtu yeyote atakayeweza kuendelea kudumu kwa kuupinga muqawama. Akaongeza: “Ikiwa bado mmebakiza hata chembe ya haya, basi rejeeni kwenye akili zenu.”
Sheikh Abdullah Al-Jabri
Kwa upande wake, Sheikh Abdullah Al-Jabri, Katibu Mkuu wa Harakati ya Ummah, alisema kuwa; kutiwa saini kwa Makubaliano ya Washington hakufikii hata thamani ya wino uliotumika kuyatia saini, ilhali damu za mashahidi bado hazijakauka.
Maoni yako